Nampenda ila kusema ngoma
Ipo nia ya kunena,
bali mie naogopa
Kwake iwe nia mbaya,
basi vipi itakuwa
Hata zaidi huenda,
moyoni kasononeka
Yeye mno namuenzi,
kwangu kusema ni ngoma
Pindi aniangalipo,
nia anayo nahisi
Siwezi jua iwapo, kawaida yake hali
Mie nimuangalipo,
nambeza kwa yakini
Yeye mno namuenzi,
kwangu kusema ni ngoma
Kutaka kunena naye,
aghalabu hunijia
Mbiombio mimi kwake,
nimfikiapo ila
Wangu mwili
wateteme, nisijue la kunena
Yeye mno namuenzi,
kwangu kusema ni ngoma
Kikomo wino natiya, naamini
ipo siku
Mrembo takuja sema,
nakupenda mwenzi wangu
Waniambiya mtima,
yenyewe ipo karibu
Yeye mno namuenzi,
kwangu kusema ni ngoma
4 comments:
vizuri kaka.
Kaka, kazi nzuri. Wewe ni malenga wa wapi?
Mwalimu wangu MUSAKALI kwa njia moja au nyingine umechangia pakubwa kwangu kuimarika maadam huenda baadhi ya mashairi yangu yaliyoko njiani nimeyatunga kutokana na semi zako darasani
USIBONYEZE KIDUDE maanake mie USTADH JOSHUA MAKORI ONGECHI ni malenga wa haiba kubwa kutoka KISII MWA KENYA
Kaka JACKSON nashukuru kwa kunitia moyo wako wa kila siku pindi ninapotoa shairi
Langu ni kukutaka wewe kuendelea kushirikiana nami na bila shaka mashairi kadhaa yapo njiani
Post a Comment