Mtima wasononeka, pindi niwazawazapo
Yale ninayoyaona, kote nijivinjaripo
Imegeuka dunia, yatisha uionapo
Jamaneni mambo gani, yameikumba dunia
Dada zanguni vyuoni, nawaomba nisikiye
Usherati mwashiriki, hamjui hatariye
Hamnazo jitieni, lakini mtajutie
Jamaneni mambo gani, yameikumba dunia
Mavazi yenu maovu, yamekosa maadili
Mwavutia dhana yenu, mngalijua laiti
Ukimwi u juu yenu, kumaliza halaiki
Jamaneni mambo gani, yameikumba dunia
Mie kikomo nafika, wakati kwangu adimu
Sitasita kuwaonya, badilika juu yenu
Lau msiposikiya, kaburini mtadumu
Jamaneni mambo gani, yameikumba dunia
6 comments:
Wewe ni malenga stadi.Nimefurahia kazi zako na naomba uendelee vivyo hivyo. asanti ndugu.
Nashukuru ndugu na natumai atakavyoridhia Maulana basi nitafanya kila juhudi kuhakikisha kwamba nimehabarisha umma kupitia njia nzima na ya kipekee ya ushairi
napenda shairi lenyewe
napenda shairi lako
sawa
basi nashukuru bwana Francis na mie nitazidi kukupekulia moja baada ya jingine kadri Mola atakavyoridhgia
Post a Comment