Nampenda ila kusema ngoma
Ipo nia ya kunena,
bali mie naogopa
Kwake iwe nia mbaya,
basi vipi itakuwa
Hata zaidi huenda,
moyoni kasononeka
Yeye mno namuenzi,
kwangu kusema ni ngoma
Pindi aniangalipo,
nia anayo nahisi
Siwezi jua iwapo, kawaida yake hali
Mie nimuangalipo,
nambeza kwa yakini
Yeye mno namuenzi,
kwangu kusema ni ngoma
Kutaka kunena naye,
aghalabu hunijia
Mbiombio mimi kwake,
nimfikiapo ila
Wangu mwili
wateteme, nisijue la kunena
Yeye mno namuenzi,
kwangu kusema ni ngoma
Kikomo wino natiya, naamini
ipo siku
Mrembo takuja sema,
nakupenda mwenzi wangu
Waniambiya mtima,
yenyewe ipo karibu
Yeye mno namuenzi,
kwangu kusema ni ngoma